Anjita Child Development Foundation imeungana na wadau wengine kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika. Maadhimisho hayo yamefanyika kwa kushirikiana na Halmashauri ya mji wa Kibaha na Umoja wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana.
Shughuli mbalimbali tulizifanya ikiwemo maandamo kuelekea shule ya Msingi Mkoani, Ugawaji wa vifaa na Zana za ujifunzaji kwa watoto wenye mahitaji maalumu.
Mgeni Rasmi alikuwa Bi. Mary Mmasi (Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Kibaha Mji). Mgeni Rashmi alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuzingatia haki za mtoto, kupinga ukatili kwa watoto, kutoa malezi bora, kufanya kazi kwa kushirikiana na kuendelea kujitoa kwaajili ya watoto wetu.




